MILIKI MLADI AMA BIASHARA YAKO!!
Je unataka mtaji ili umiliki Mradi au Biashara yako ? Soma hapa kuna suluhisho.
tangazo hapa
Je unataka mtaji umiliki Biashara yako?Mtaji ni nini?
Ni kitu chochote ambacho unaweza kutumia katika kuzalisha kitu kingine kwa lengo la kupata faida.(kianzio).mfano mtaji wa Mc ni nguo nzuri au kubwa nadhifu,nauli ya kufika eneo la tukio.
Mtaji sio Pesa pekee kama jinsi watu wanavyozani Bali pia unaweza ukawa na akili au wazo la Biashara.unaweza toa wazo na wenzako wakatoa Pesa.mfano mtu una uwezo wa kutengeneza sabuni mbalimbali, batiki,chaki wewe ukatoa wazo/ujuzi mwenzio wakatoa Pesa /msingi mkauza mkagawana faida,mwisho wa Siku ukatimiza ndoto zako.
Jinsi ya kupata mtaji ili uanzishe mradi wako.
1.Unaweza ukafanya Biashara za mtandao .
2.Kufanya makubaliano na mtu anaezalisha kitu Fulani ukatafuta mteja kwa njia yoyote alafu ukalipwa na wewe unapata asilimia Fulani mwisho wa Siku utakuza mtaji.mfano Gabriela sandels and bag
3.Kutumia ubunifu uliosoma darasani na kuifikishia jamii.Kuna wasomi wengi wanalalamika hakuna ajira huku wamezilalia shahada zao kwa mfano wewe ni mtalaamu wa mambo ya Computer wafundishe watu masomo ya computer kwa gharama nafuu kwa mfano fundisha jinsi ya kutengeneza blog,website, application mbalimbali tembelea maofisi na kujitambulisha na utengeneze program mbalimbali za kiofisi.wewe kama mchumi wafundishe watu maswala ya uchumi,andiko mradi etc
4.Mikopo kutoka taasisi za fedha.mfano bank,Sacco's,vicoba
5.Kuuza Mali unazomiliki mfano shamba
6.Uwekaji wa akiba,Jamani hakuna uchawi mzuri na wenye mafanikio kama uchawi wa kuweka akiba unaweza weka akiba bank ,ukanunua hisa etc .waswahili husema akiba haiozi kwahiyo jinyime Leo kwa mafanikio ya baadae.Watu wengi tunamatumizi mabaya mfano unamkuta mama anamanguo kibao na mwengine havai lakini kila wiki anendelea kununua nguo ananunua havai anarundika ndani kwasababu ameipenda.
7.Mtaji kutokana na ufadhili.ufadhili huu unaweza ukawa kutoka serikalini,watu binafsi,ufadhili kutoka nje ya nchi.ufadhili huu hutolewa kwa vikundi ,Asasi za kiraia na vicoba .Ni lazima mjisajiri halmashauri husika /Brela Pesa zipo nyingi na umoja ni nguvu.
8.Kibati ,ni chanzo cha mtaji kisichohitaji gharama ili kupata mtaji unaweza anzisha vikundi vya kuchangiana kwa njia ya mzunguko mfano unahitaji mtaji wa 100000 kila mwezi lazima watu 10 wachangie 10000.
Kwanini watu wanakosa mtaji?
1.Hawatumii vipaji vyao walivyopewa na maanani mfano mtu una elimu ya kuandika andiko mradi na Wafanyabiashara wengi wanaitaji waandikiwe ili wapate mkopo bank wewe umeikalia elimu hiyo.
2.Ubinafsi.Mtu anaweza kuwa na kipaji Fulani mfano kutengeneza Blog anashindwa kufundisha wenzake hata kwa Pesa anabaki kuikalia tu,vile vile watu hawapendi kufanya kazi kwa vikundi kila mtu anataka afanikiwe peke yake mwisho wa Siku Pesa za misaada zipo wakupewa hawaonekani.
3.Uvivu.kuna watu wengine wamebobea katika mambo ya kilimo ni mtaalam ana shahada ,astashahada au cheti lakini kwake hata kibustani cha mfano hakuna.kumbe ukifanya hivo unaweza pata majirani na wao wakahitaji Huduma zako mwisho ukapata mtaji.
4.Watu kupenda kufanikiwa haraka.Mtu yuko radhi abeti ,afanye online donation ili apate Pesa nyingi kwa haraka kuliko kufanya mradi wenye mafanikio kwa mda mrefu.
Maoni 0:
Chapisha Maoni
Zingatia: Mwanachama wa blogu hii tu ndiye anayeweza kuchapisha maoni.
Jisajili kwenye Chapisha Maoni [Atom]
<< Nyumbani